REVOLUTIONARY GOVERNMENT OF ZANZIBAR

MINISTRY OF AGRICULTURE, IRRIGATION, NATURAL RESOURCES AND LIVESTOCK

NEWS AND EVENTS


60% Complete (warning)
  • 2024-04-15
  • KATIBU MKUU AWAHIMIZA WAKULIMA KUTUNZA MICHE NA VIFAA VYA ZAO LA KARAFUU

    Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Ali Juma Khamis amewataka Wakulima wa Mikarafuu kutunza miche na Vifaa wanavyopewa ili lengo la kukuza Uzalishaji wa Zao hilo liweze kufikiwa.

    Hayo ameyasema huko Ofisini kwake Maruhubi Wakati wa Makabidhiano ya Vifaa vya Uzalishaji Miche ya Mikarafuu.

    Amesema Lengo la Utoaji wa vifaa hivyo ni kutokana na Mashirikiano yaliopo na ZSTC katika kuwasaidia Wakulima wa Zao hilo katika kuthamini Mchango wa Sekta ya

    Read More
  • 2024-04-09
  • SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUENDELEA KUIMARISHA MASHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KUKUZA KILIMO BORA ZANZIBAR

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuimarisha Mashirikiano na Mashirika ya Maendeleo na Binafsi katika kuongeza Uwezekezaji ambao utasaidia kuwa na kilimo endelevu na Chenye tija.

    Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis ameeleza hayo wakati alipofungua Kikao cha Mkakati wa Majumuisho ya Uwezekezaji katika mazao ya Maziwa na Mwani huko katika Ukumbi wa ZURA.

    Shamata alisema fursa za Uwekezaji zilizomo katika Mnyororo wa

    Read More
  • 2024-03-24
  • SERA YA KILIMO KUSAIDIA KUSIMAMIA UZALISHAJI WA MAZAO

    Katibu Mkuu kiongozi wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhandisi Zeyna Ahmed Said amesema kuwepo kwa Sera ya kilimo kutasaidia kusimamia uzalishaji wa mazao na kuleta mabadiliko ya Sekta ya kilimo. AKIZUNGUMZA katika ukumbi wa ZURA Maisara wakati akifungua kikao cha kupitia Sera ya Kilimo na kupokea maoni kwa Makatibu wakuu na Manaibu katibu wa Mawizara ya Serekali ya Mapinduzi Zanzibar.


    Amesema kilimo kina umuhimu Mkubwa katika kuchangia pato la nchi ambapo

    Read More
  • 2024-03-21
  • WAZIRI WA KILIMO SHAMATA SHAAME KHAMIS ASEMA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA MISITU LIBAKI KWA WANANCHI.

    Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis amesema jukumu kubwa la usimamizi wa Rasilimali za Misitu linabaki kwa Wanachi kwani wao ndio watumiaji wakubwa wa rasilimali hizo.

    Shamata aliyasema hayo huko katika Maadhimisho ya siku ya Misitu duniani yaliyofanyika Jozani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

    Alisema jambo hilo litakuwa la busara ikiwa Wananchi wenyewe wataendelea kuilinda, kuitunza na kuihifadhi Misitu kwa vile kukosekana kwake wao

    Read More
  • 2024-04-09
  • KATIBU ALI KHAMIS ASEMA USHIRIKISHWAJI WA JAMII NI NJIA PEKEE YA USIMAMIZI WA MISITU

    Katibu Mkuu Wizara ya kilimo,Umwangiliaji,Maliasili na Mifugo Ndg: Ali Khamis Juma Amesema ushirikiswaji wa jamii katika kutoa maoni yao ndio njia pekee itakayo saidia usimamizi mzuri wa misitu ya hifadhi.

    Akizungumza katika kikao cha mpango kazi wa usimamizi wa Msitu wa akiba wa Kidikotundu, Nongwe na Vundwe kilichowashirikisha wa wadau kutoka tasisi za Serekali na binafsi,wasimamizi wa misitu,wanyama pori na wanajamii kutoka Mkoa wa Kusini Unguja.


    Amesema

    Read More
  • 2024-03-19
  • WANAFUNZI WAPATA ELIMU YA MISITU KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA MISITU DUNIANI 2024

    Msaidizi Mkuu wa Hifadhi ya Kimaumbile ya Masingini Amour Khamis Juma amesema ipo haja kwa Jamii na Wanafunzi kuwashirikisha katika utoaji wa Elimu ili kujua umuhimu wa Misitu na kutambua rasilimali zilizopo ikiwemo wanyama, ndege na miti adimu sambamba na kuhifadhi mazingira kwa ujumla.

    Hayo ameeleza huko katika hifadhi ya kimaumbile ya masingini wakati alipokua akitoa elimu kwa wanafunzi wa skuli ya Mtoni Kigomeni, skuli ya Bububu ‘A’ na Mtopepo ‘B’ kwa kuelekea

    Read More
  • 2024-03-16
  • WAZIRI SHAMATA ATEMBELEA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI MAJI CHEJU

    Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Mheshimiwa Shamata Shaame Khamis amemtaka Mkandarasi anaehusika na Ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji maji ikiwemo Uchimbaji na utengenezaji wa Visima katika bonde la Cheju B kuhakikisha Ujenzi unamaliza kwa wakati ili Wakulima waweze kurudi katika mabonde yao na kuendelea na kilimo.

    Hayo ameyasema huko bonde la Cheju B Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni Ziara ya kuangalia Ujenzi unaoendelea kujengwa ktk bonde hilo

    Amesema

    Read More
  • 2024-03-14
  • SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR ITASHIRIKIANA NA WADAU WA KIMAENDELEO KATIKA TAFITI

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Wadau wa kimaendeleo katika tafiti kwa nia ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya mboga mboga na kuwajengea Uwezo Wakulima ili Kuongeza kasi ya Uchumi Nchini.

    Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ZARI Dkt. Mohamed Dhamir Kombo ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Taasisi hiyo Kizimbani wakati alipofungua Mafunzo kwa Wakulima ya Uzalishaji wa mbegu bora za mboga mboga.

    Alisema Serikali imepiga hatua kubwa

    Read More
  • 2024-03-14
  • MAJAA MITAANI YAZIDISHA ONGEZEKO LA MBWA

    KUWEPO kwa majaa mengi ya taka kumetajwa kuwa ni miongoni mwa mambo yanayochangia kuwepo kwa mbwa wengi mitaani hali inayosababisha baadhi ya mbwa kukosa tiba ya chanjo kwa wakati kutokana na kutokua na wamiliki.

    Akitoa taarifa ya chanjo ya kichaa cha mbwa iliyotolewa na Idara ya Maendeleo ya Mifugo, Daktari Mkuu wa wanyama katika idara hiyo, Dk. Ali Zahran Mohamed, alisema kwa mwaka huu idara yake imeendesha zoezi la uchanjaji na mbwa wapatao 3,616 walipatiwa huduma hiyo katika

    Read More
  • 2024-03-14
  • SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YAWASHAURI WAKULIMA KUJIANDAA NA MSIMU WA MASIKA

    Kufuatia Utabiri wa Hali ya Mvua kwa kipindi cha Masika 2024, Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo imewashauri Wakulima kuandaa mashamba, kupanda, kupalilia pamoja na kutumia Pembejeo kwa wakati ili kuepuka athari za mvua ya Masika zinazotarajiwa kunyesha katika Visiwa vya Zanzibar.

    Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Sera na Utafiti, ndugu Makame Kitwana Makame huko katika Ukumbi wa Wizara hiyo Maruhubi wakati alipokua akijadili na Wakurugenzi pamoja na

    Read More
  • 2024-03-14
  • SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YARUHUSU UINGIZAJI WA NDIZI

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeruhusu uingizwaji wa zao la ndizi nchini sambamba na kuchukua tahadhari juu ya magonjwa mbali mbali yanayoathiri zao hilo

    Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Shamata Shaame Khamis, ametoa rai hiyo huko katika ukumbi wa wizara hiyo Maruhubi wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya uingizwaji wa zao la ndizi nchini kwa tahadhari maalum.


    Alisema mwaka 2007 Serikali ilitangaza marufuku ya kutoingiza mmea wa

    Read More