REVOLUTIONARY GOVERNMENT OF ZANZIBAR

MINISTRY OF AGRICULTURE, IRRIGATION, NATURAL RESOURCES AND LIVESTOCK

ABOUT US


60% Complete (warning)
BACKGROUND

Historia ya Maendeleo ya Kilimo Zanzibar imeanza katika mwaka 1895 wakati Serikali ya Zanzibar Chini ya Himaya ya Uingereza ilipoundwa Idara ya kilimo iliyoitwa Idara ya Ziraa na Makao Makuu yake yalikuwa Dunga kwa Mwinyi Mkuu au Jumba la Mawe.

Idara hiyo ilifungua vituo Machui na Kinooni kwa lengo la kueneza kazi zake. Mwaka 1934 Kituo cha Utafiti Kizimbani kilifunguliwa hii ilitokana na kuwa hali ya hewa ya eneo hilo ni nzuri, lenye muinuko na udongo wa aina moja. Madhumuni ya kituo hicho ni kufanya utafiti wa mikarafuu.

Kuanzishwa Wizara ya Kilimo.

Historia ya Wizara ya Kilimo inaonesha kuwa kuanzishwa kwake kumetokana na kutanuka kwa kazi za Idara hii ya Kilimo iliyoanzishwa Mwaka 1895 na ilijulikana kama Wizara ya Kilimo na Maliasili ili kuingiza na Sekta ya Misitu.

Mwaka 1934 kilifunguliwa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani kwa sababu mahala hapo palionekana kuwa na hali ya hewa nzuri kwa vile ni eneo lenye muinuko na lenya udongo unaofanana. Madhumuni ya kituo hicho kwa wakati ule ni kufanya utafiti wa mazao ya biashara hasa mikarafuu ili kukuza uzalishaji wa zao hilo, pamoja na kuatika miche ya minazi. Serikali ya kikoloni iliamini kuwa Zanzibar haiwezi kujitosheleza kwa chakula na kwa hivyo wafanyabiashara walipewa fursa ya kununua mazao ya karafuu, mbata na pilipili kichaa kwa kusafirisha ili waagize chakula.

Karafuu ndio zao kuu la kiuchumi lilotegemewa zaidi, hata hivyo, hatari ya kutegemea zao moja kwa uchumi ilionekana ambapo umuhimu wa kufanya tafiti ya kupata mazao mengine ya biashara zilianza tokea mwaka 1860. Mazao yaliofanyiwa utafiti (Taftish) kwa wakati ule yalikuwa ni Mpira, Vanila, Cacao, Buni, Chai, Pilipili kichaa na Miwa. Mazao hayo mengi hayakuonesha matumaini ya kuinua uchumi wa Zanzibar, kati ya mwaka 1950 na 1960 utafiti wa mazao mengine uliendelea kwa mazao ya viungo, ndimu, Mllangilangi, Zingifuri na Pamba. Pamoja na juhudi hizo karafuu bado imeendelea kubakia kuwa zao la kutegemewa kibiashara.

MISSION

DHIMA YA WIZARA YA KILIMO

Kutayarisha na kusimamia kazi na miradi ya kilimo, sambamba na matumizi ya teknolojia za kisasa, kuongeza uzalishaji na tija kupitia mpango endelevu ili kuwezesha uzalishaji, kutoa huduma zitakazosaidia wakulima pamoja na kuhakikisha matumizi endelevu ya maliasili.

VISION

DIRA YA WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI

Dira kuu ya Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar ni kuleta maendeleo endelevu ya sekta ya kilimo na kukifanya kiwe cha kisasa na tija kwa ajili ya faida za kiuchumi, kijamii na kimazingira ifikapo mwaka 2025.

CORE VALUES

LENGO KUU LA WIZARA

Kuimarisha utendaji na usimamizi wa sekta kwa kuongeza wigo wa mapato, uzalishaji na tija kwa mazao ya chakula, biashara, mifugo na kushajiisha uwekezaji katika teknolojia na miundombinu ya uzalishaji na uanzishwaji wa viwanda. Wizara pia inalenga kushajiisha uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu. Sekta ya Kilimo kwa sasa inajumuisha sekta ndogo za mazao, mifugo na misitu bado inaendelea kuwa ni muhimili mkuu wa uchumi wa Zanzibar na inatoa mchango wa moja kwa moja katika kujikimu kimaisha ambapo inatoa ajira rasmi kwa wastani wa asilimia 40; na zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wanategemea sekta hii kwa njia moja au nyengine katika kujipatia kipato na kuimarisha maisha yao.