Event Details
Photo

Posted: 2025-05-20

WAZIRI WA KILIMO UMWAGILIAJI MALIASILI NA MIFUGO MHE. SHAMATA SHAAME KHAMIS ASHIRIKI KATIKA UPANDAJI MITI KWA MAAZIMISHO YA SIKU YA MISITU DUNIA.

Description

Serikali itaendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa jamii juu ya suala zima uhifadhi wa misitu na upandaji wa miti

Ameyaeleza hayo Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis alipokuwa katika madhimisho ya siku ya misitu Duniani yalioyofanyika Bumbwini Mkoa wa Kaskizini Unguja.

Amesema ni vyema jamii kushirikiana kwa pamoja katika uhifadhi wa misitu kwani hupelekea kuboresha mazingira na kutunza vyanzo vya maji na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Ameeleza iwapo jamii itatunza misitu na kuendeleza upandaji wa miti itapelekea kulinda mmong\'onyoko wa mwambao ya bahari na kupunguza ongezeko la joto linalochangia kuibuka maradhi mbali mbali Aidha amesema uwepo wa misitu hupelekea ongezeko la watalii na wawekezaji ikiwemo ufugaji wa kaa wa njia za kisasa katika maeneo ya Zanzibar.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo amesema Wizara imejipanga kuandaa mpango shirikishi na kamati za mazingira utakao simamia uhifadhi wa mazingira katika maeneo yanayoizumgunga hifadhi za Misitu.

Vile vile, ameeleza kuwa Serikali ina malengo ya kutoa elimu ambayo itashajihisha jamii kuhifadhi mazingira ili kuacha ukataji wa miti ovyo.

Nae mratibu wa Matembezi ya Uhisani kutoka Kigoma Jiji Philip John yanayoshajihisha upandaji wa misitu.

Amesema kupitia Matembezi hayo wamefanikiwa kutoa elimu katika mikoa tofauti ya Tanzania ikiwa Ina lengo la kushajihisha jamii upandaji wa miti ili kutunza mazingira kwa faida ya kizazi Cha sasa na baadae Sambamba na hayo wamewasisitiza vijana kutunza mazingira ili isipoteze uhalisia wake na kuangana mkono kwa pamoja katika utunzaji wa mazingira.

Maazimisho ya siku ya misitu Dunia hufanyika Kila tarehe 21 Machi kwa upande wa Zanzibar imebeba kauli mbiu \"Hifadhi Misitu ili isishe Zanzibar ya kijani \"

Follow Us