WAZIRI AKUTANA NA WATENDAJI WA WIZARA KILIMO-March 2019

WAZIRI WA KILIMO MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI MHE MMANGA MJENGO MJAWIRI AMEWATAKA WAFANYAKAZI WA WIZARA HIYO KUWEZA KUBUNI MBINU MBALIMBALI ZA KITAALAMU KATIKA SEKTA YA KILIMO ILI KUWEZA KUFANYA KAZI KWA UFANISI ZAIDI NA KULETA MABADILIKO NDANI YA SEKTA HIYO NA JAMII KWA UJUMLA. AMEYASEMA HAYO WAKATI ALIPOKUA AKIZUNGUMZA NA WAKUU WA VITENGO VILIOMO NDANI YA WIZARA HIYO PAMOJA NA WAFANYAKAZI MBALIMBALI HUKO KATIKA UKUMBI WA ASSP MARUHUBI ILI KUONA KUA SEKTA YA KILIMO INAKUA NA WANANCHI KUWEZA KUNUFAIKA KWA KUITUMIA SEKTA HIYO. AMEFAHAMISHA KUA SEKTA YA KILIMO NI SEKTA MUHIMU SANA KATIKA MUHIMILI WA NCHI NA INAFANYAKAZI KWA JAMII ZAIDI HIVYO WAFANYAKAZI HAWANA BUDI KUFANYA KAZI KWA UFANISI ZAIDI NA KUITUMIA ELIMU WALIYONAYO KWA FAIDA YA JAMII NA KUWAFIKIA WAKULIMA KWA VILE SEKTA HII INALENGA ZAIDI WAKULIMA AMBAO WANAJISHUHULISHA NA SHUHULI ZA UZALISHAJI WA MAZAO. AIDHA ALIWATAKA WAFANYAKAZI HAO KUWFANYAKAZI KWA NIDHAMU NA KUTII AMRI, SHERIA,MIONGOZO NA KANUNI ZA KAZI NA KUWA NA MASHIRIKIANO AMBAYO YATASAIDIA KUTAMBUA MAPEMA MAPUNGUFU NA CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA SEHEMU ZA KAZI NA KUWEZA KUZITAFUTIA UFUMBUZI WAKE. NAE NAIBU WAZIRI WA KILIMO,MALIASILI MIFUGO NA UVUVI MHE: DR. MAKAME ALI USSI AMEWASISITIZA WAFANYAKAZI HAO KUWEZA KUJIKUBALISHA KATIKA MAJUKUMU YAO YA KAZI ILI MALENGO AMBAYO WIZARA IMEJIPANGIA YAWEZE KUFIKIWA.