WIZARA YA KILIMO YAKABIDHI DHANA ZA KILIMO KWA WAKULIMA-March 2019

WAZIRI WA KILIMO MALIASILI,MIFUGO NA UVUVI MHE.MMANGA MJENGO MJAWARI AMEKABIDHI JUMLA YA MASHINE 3 ZA KUCHIMBIA NA KUBURUGIA MPUNGA (POWER TILLER) KWA JUMUIYA ZA WAKULIMA WA MPUNGA WA UMWAGILIAJI MAJI HUKO MTWANGO WILAYA YA MAGHARIB B. GHAFLA HIYO ILIYOFANYIKA KATIKA BONDE LA MTWANGO WILAYA YA MAGHARIBI ‘’B’’ ILIWASHIRIKISHA WAKULIMA WA JUMUIYA ZA MABONDE YA BUMBISUDI,MTWANGO NA UZINI ILI KUWEZA KUENGEZA NGUVU KATIKA KAZI YA KILIMO NA KUZIDISHA KASI YA UZALISHAJI WA MPUNGA NCHINI. AMEFAHAMISHA KUA UTOAJI WA VIFAA UMETOKANA NA JUHUDI KUBWA ZINAONESHWA NA WIZARA YA KILIMO MALIASILI KILIMO NA UVUVI KWA WAKULIMA WAKE ILLI WAWEZE KUENDANA NA MABADILIKO YA DUNIA KWA MKULIMA KUWEZA KUTUMIA TEKNOLIJIA MPYA NA KULIMA KWA UFANISI ZAIDI. AMESEMA KUA WIZARA IMEPEWA JUKUMU LA KUENDELEZA SHUGHULI ZA KILIMO HASA KATIKA KUTOA HUDUMA NA VIFAA VYA KILIMO PAMOJA NA KUWAPATIA WAKULIMA WATAALAMU WA KILIMO HASA KATIKA KILIMO CHA MPUNGA WA UMWAGILIAJI MAJI NA KUENGEZA KASI YA UZALISHAJI. AIDHA AMEWATAKA WAKULIMA HAO KUWEZA KUVITUNZA VIFAA HIVYO ILI VIWEZE KUFANYA KAZI KWA MUDA MREFU KWANI WIZARA IMEJIPANGA KUWASAIDIA WAKULIMA KWA KILA HALI ITAPORUHUSU ILI LENGO LA KUJKIMU KATIKA KILIMO LIWEZE KUFIKIWA NAE MKURUGENZI IDARA YA KILIMO HAJI HAMID SALEH AMEFAHAMISHA KUWA KWA SASA UZALISHAJI WA MPUNGA KWA NJIA YA UMWAGILIAJI MAJI UMEENGEZEKA KWA MKULIMA KUWEZA KUPATA GUNIA KUMI NA TANO KWA ROBO EKA TOFAUTI NA KIPINDI CHA NYUMA JAMBO AMBALO LINATIA FARAJA KWA WAKULIMA HAO. AMEFAHAMISHA KUA SERIKALI KUPITIA MRADI WA KUONGEZA UZALISHAJI NA TIJA KKWENYE KILIMO CHA MPUNGA WA UMWAGILIAJI MAJI [ERPP] UMEWEZA KUSAIDIA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI MAJI AMBAPO ZAIDI YA WAKULIMA MIA TANO TISINI NA NANE 598 WAMEWEZA KUNUFAIKA NA HUDUMA HIYO. AKISOMA RISALA KWA NIABA YA WAKULIMA WENZAKE KATIBU WA JUMIA YA WAKULIMA WA BONDE LA MTWANGO OTHMAN ZAHOR ABDALLA AMEUSHUKURU UONGOZI WA WIZARA YA KILIMO MALIASILI MIFUGO NA UVUVI KWA KUWAPATIA VIFAA HIYO AMBAVYO VITAWAWEZESHA KUFANYA KAZI KWA UFANISI ZAIDI. HATA HIVYO AMEFAHAMISHA KUA INGAWA SERIKALI INAWAPATIA HUDUMA HIZO WAMEIOMBA WIZARA HUSIKA KUWAPATIA WATAALAMU WA KUTOSHA ILI WAWEZE KULIMA MARA TATU KATIKA MSIMU WA KILIMO AMBAPO KWA SASA WANALIMA MARA MBILI KWA MSIMU. VIFAA HIVYO VILIVYOTOLEWA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUPITIA WIZARA YA KILIMO MALIASILI MIFUGO NA UVUVI NI MSAADA KUTOKA SEREKALI YA KUWEIT AMBAPO JUMLA YA MASHINE SITA 6 ZIMETOLEWA KWA MGAWANYO WA PEMBA NA UNGUJA KWA LENGO LA KUKUZA KILIMO CHA MPUNGA WA UMWAGILIAJI MAJI NA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UAGIZAJI WA CHAKULA KUTOKA NJE YA NCHI.